Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islām wal-Muslimīn Sayyid Ahmad Ali Abidi, Imamu wa Ijumaa wa Mumbai na mwakilishi wa Ayatollah al-‘Uzmā Sayyid Ali Sistani nchini India, kufuatia ushindi wa kihistoria wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya uvamizi wa utawala wa Kizayuni na Marekani, katika ujumbe wake, amepongeza ushindi huo kwa Umma wa Kiislamu, hasa kwa wafuasi wa Ahlul-Bayt (as), na akautaja kuwa si ushindi wa kijeshi tu, bali ni nembo ya imani, hamasa ya kishujaa na kusimama kidete mbele ya ubeberu wa dunia.
Katika ujumbe huo amesema kuwa:
"Huu ni mwanzo tu wa njia; mwisho wa mapambano haya bado haujafika, na kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, siku hiyo pia haiko mbali ambapo uasi na dhulma vitang’olewa kabisa."
"Leo hii, Iran ya Kiislamu imevunja majivuno na kiburi cha utawala wa Kizayuni ambacho kwa miaka mingi kilikuwa kivuli cha dhulma juu ya wanyonge. Madhehebu ya Kishia, si tu kwamba yameitetemesha dola hii dhalimu, bali pia yamelegeza misingi ya utawala wake. Tunawaombea dua mashujaa waliowapiga pigo hili la mauti – Mwenyezi Mungu awalinde na awalipe ujira mkubwa."
Mwanazuoni huyu mashuhuri wa India, akigusia pia kusimama kwa ujasiri kwa Iran mbele ya Marekani, alisema:
"Kama ambavyo kiburi cha Israel kimeporomoshwa ardhini, vivyo hivyo, fahari ya Shetani Mkuu—Marekani—nayo pia imevunjwa. Lakini jambo la kusikitisha ni kuwa tawala hizi zimefikia kiwango cha juu cha kufuru na kujivuna kiasi kwamba hazijifunzi chochote kutokana na kushindwa kwao, wala hawahisi aibu yoyote."
Maoni yako